Tahadharini kwelikweli juu ya mfumo huu unaoanza kuenea kati yetu. Wanadai ukati na kati. Hii leo kuna wenye kusema:

“Ninaenda kwa Ahl-us-Sunnah na Salafiyyuun na kuchukua elimu kutoka kwao. Kisha naenda kwa Ahl-ul-Bid´ah na kuchukua elimu kutoka kwenye makundi mengine mbali na Salafiyyuun.”

Kuna mmoja katika maimamu wa waislamu aliulizwa juu ya mtu kama huyu na akatoa jawabu la kutosha. Kulisemwa kuambiwa al-Awzaa´iy juu ya mtu anayesema kuwa anakaa na Ahl-us-Sunnah na anakaa vilevile na Ahl-ul-Bid´ah. al-Awzaa´iy akasema:

“Huyu ni mtu anayetaka kusawazisha haki na batili.” al-Ibaanah al-Kubraa (2/456).

Ibn Battwah amesema alipokuwa anayawekea taaliki maneno haya:

“al-Awzaa´iy amesema kweli. Mtu huyu hapambanui kati ya haki na batili wala kufuru na imani.”

Tahadharini kwelikweli kukaa na Ahl-ul-Bid´ah. Tahadharini kwelikweli juu ya kudanganyika na elimu yao. Yaliyoko kwa Ahl-us-Sunnah ni mengi na masafi zaidi.

Walio na mfumo huu mbaya wajifunze kutoka kwa ´Imraan bin Hittwaan aliyemuoa binadamu yake ambaye alikuwa ni katika Khawaarij. Lengo lake ilikuwa ni kumtengeneza na kumwongoza, lakini mwanamke huyu akamfanya kuwa katika Khawaarij waliopindukia!

Wapate mazingatio kutoka kwa Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy aliyesema:

“Marafiki zangu kutoka katika Hanaabilah walikuwa wanataka niwasuse wanachuoni wengi, nilikuwa naona kuwa hilo linanizuia na elimu yenye manufaa.”

Hivi ndivyo anavyosema Ibn ´Aqiyl – Allaah amsamehe. adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) anayatilia taaliki maneno haya na kusema:

“Walikuwa wanamkataza kukaa na Mu´tazilah, anakataa. Hatimae akatumbukia katika mtego wao na akawa na ujasiri wa kuyapotosa maandiko ya Qur-aan na Sunnah. Tunamuomba Allaah usalama.” Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (19/447).

Huu ndio mwisho wa mfumo huu wa kati na kati ambao haukujengwa juu ya Qur-aan, Sunnah na mfumo wa Salaf (Rahimahumu Allaah).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 68-70
  • Imechapishwa: 09/08/2020