Wanachuoni wamefautiana watu wakiuona mwezi katika mji, inawalazimu watu wote ulimwenguni kufunga au hapana?

Maoni ambayo yanatambulika kwa Imaam Ahmad na wafuasi wake ni kwamba ni wajibu kwa waislamu wote ulimwenguni kufunga. Kwa sababu Ramadhaan imethibiti kuingia kwake na imethibiti hukumu yake na hivyo ni wajibu kufunga. Ni miongoni mwa mambo ambayo Ahmad amepwekeka nayo. Ndio madhehebu ya Abu Haniyfah vilevile.

Wapo wanachuoni wengine ambao wanaona kuwa si wajibu na kwamba kila nchi wana mwandamo wao. Hayo ndio maoni ya al-Qaasim bin Ahmad, Saalim bin ´Abdillaah na Ishaaq…

ash-Shaafi´iy akafafanua zaidi kama inavyojulikana kutoka kwake. Wamesema ikiwa kunatofautiana kwa mwandamo wa mwezi, basi kila watu wana hukumu ya kuandama kwao. Na ikiwa mwandamo wa mwezi unaafikiana, basi hukumu yao itakuwa moja katika kufunga na kufungua. Hili ndilo chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab bin al-Marraakshiy  amesema katika kitabu chake “al-´Adhb-iz-Zilaal fiy mabaahith Ru´yat-il-Hilaal” ya kwamba ikiwa kati ya miji miwili kuna masafa ya 2226 km basi mwezi wao utakuwa mmoja. Zaidi ya hapo hapana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Bassaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-´Allaam Sharh ´Umdat-il-Ahkaam, uk. (01/315-316)
  • Imechapishwa: 14/05/2018