Mwenye mimba anasoma du´aa ya kujilinda na shaytwaan kabla ya jimaa?


Swali: Mwanamke akiwa na mimba. Imewekwa katika Shari´ah kuomba du´aa:

بسم الله اللهم جَنِّبْنَا الشَّيْطَانَ وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا

“Kwa jina la Allaah. Ee Allaah! Tulinde na shaytwaan na kilinde na shaytwaan kile unachoturuzuku.”?

Au hili ni jambo maalum linalofanywa kabla ya mimba?

Jibu: Si jambo maalum. Ni jambo lenye kuenea. Mimba haitakiwi kulindwa dhidi ya shaytwaan? Mjamzito hatakiwi kumuomba Allaah amlinde kutokamana na shaytwaan?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 30/06/2018