Mwenye maradhi ya chembe ya moyo na kuvuja damu kwa ndani na twahara

Swali: Tangu utotoni mwangu nilikuwa naishi na chembe ya moyo na kuvuja damu kwa ndani:

1 – Je, nina thawabu juu ya hilo kwa sababu nimekosa ujana wangu na afya yangu?

2 – Mara nyingi huswali kwa Tayammum kwa sababu siwezi kuoga. Je, inafaa kwangu kufanya hivo?

3 – Je, naweza kuwafunza wanafunzi Qur-aan pasi na twahara?

Jibu:

1 – Ukifanya subira kwa yale yaliyokupata basi unapata thawabu mbele ya Allaah. Ukikata tamaa na usisubiri basi unanyimwa thawabu.

2 – Ukweli wa mambo ikiwa ni vile ulivosema kwamba huwezi kuoga, basi imesuniwa kwako kufanya Tayammum kutokana na janaba.

3 – Ikiwa huwezi kutumia maji katika twahara kutokana na hadathi, basi itakutosha kufanya Tayammum kwa ajili ya twahara kwa ajili ya kugusa msahafu. Baada ya hapo itafaa kwako kufunza Qur-aan ijapo utakuwa huna twahara kutokana na hadathi ndogo.

Kuhusu mwenye janaba haifai kwake kugusa msahafu, asisome Qur-aan na wala asiwafunze wanafunzi mpaka kwanza atwahirike.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (05/380) nr. (8592)
  • Imechapishwa: 05/06/2022