Amesema (Ta´ala):

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Hawakuamrishwa [chochote kile] isipokuwa wamwabudu Allaah kwa kumtakasia Yeye dini, kuwa na imani ilio safi na wasimamishe swalah na watoe zakaah – na hiyo ndiyo dini iliyosimama imara.” (98:05)

Dini haiwi imara isipokuwa kwa kupatikana imani na matendo mema aliyoamrisha Allaah. Allaah Amjaze mwandishi – Imaam al-Aajurriy – kheri kwa kusilimulia dalili nyingi na mapokezi kutoka kwa maimamu wa Uislamu ili aweze kumkinaisha yule mwenye kutafuta haki juu ya kwamba huu ndio mfumo sahihi. Hii ndio ´Aqiydah salama inayofahamishwa na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) na maimamu hawa wa Uislamu wakajitahidi – radhi za Allaah ziwe juu yao na Awarehemu rahmah iliyo kunjufu. Hakika wao ndio maimamu wa uongofu na Allaah Anawaongoza watu kupitia wao. Hivyo basi, shikamaneni na mfumo wao. Huku ndio kufuata njia wa waumini na yule mwenye kwenda kinyume nayo anaangamia.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (2/41)
  • Imechapishwa: 26/08/2020