Mwenye kutubia tawbah ya kweli Allaah anamsamehe hata kama hakuhiji

Swali: Mtu akiwa na madhambi makubwa kisha akahiji Allaah huyafuta madhambi haya baada ya kutubia?

Jibu: Mtu akitubia juu ya madhambi yake, ijapokuwa hatahiji, midhali tawbah aliyotubia ni ya kweli, basi Allaah anamfutia madhambi yake. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ

“Wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mungu mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah ameiharamisha isipokuwa kwa haki na wala hawazini – na atakayefanya hivyo… “

Bi maana yule mwenye kumshirikisha Allaah, akaiua nafsi au akazini:

يَلْقَ أَثَامًا يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ

“… atakutana na adhabu. Ataongezewa adhabu maradufu siku ya Qiyaamah na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akafanya matendo mema, basi hao Allaah atawabadilishia maovu yao kuwa mema.”[1]

Wewe ukitubu tawbah ya kweli, hata kama hukuhiji, basi Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anayafuta madhambi yako.

[1] 25:68-70

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/964
  • Imechapishwa: 20/05/2020