Mwenye kuswali kwa kulala ni lazima aelekee Qiblah?


Swali: Ni lazima kwa mgonjwa ambaye anaswali kwa kuelekea Qiblah aelekeze uso wake Qiblah?

Jibu: Ndio, ni lazima. Kuelekea Qiblah ni miongoni mwa masharti ya kusihi kwa swalah. Ni lazima aelekeze uso na mwili wake Qiblah. Aswali kwa kulalia ubavu na huku ameelekeza uso na mwili wake Qiblah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (46) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2152
  • Imechapishwa: 06/09/2020