Mwenye kusoma Qur-aan na Adhkaar anaweza kurogwa?

Swali: Uchawi unaweza kumpata mtu ambaye anasoma Adhkaar za asubuhi na jioni na za wakati wa kulala  na kusoma Qur-aan?

Jibu: Mara nyingi mtu akizisoma kwa kuhudhurisha moyo… bali uhakika wa mambo ni kwamba hasibiwi. Mtu akisoma Adhkaar kwa kuhudhurisha moyo, kumuamini Allaah (´Azza wa Jall) na kumtegemea Allaah hali ya kuwa na yakini hasibiwi. Ama akizitumia hali ya kughafilika au si mwenye kuamini kwa kukata kuwa zinanufaisha, bali anaona kuwa huenda zikamfaa kweli kama ambavo huenda zisimfai, huyu anasibiwa. Kwa sababu hakumtegemea Allaah na wala hakuamini kuwa Adhkaar hizi zitamzuia na yachukizayo. Yakini na kumtegemea kwake Allaah kumedhoofika. Huyu anasibiwa. Ama yakini yake ikiwa na nguvu na kumtegemea Kwake Allaah (´Azza wa Jall), hatosibiwa kabisa. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

“Yeyote anayemtegemea Allaah, basi Yeye humtosheleza.”[1]

Hii ni ahadi kutoka kwa Allaah (Ta´ala).

[1] 65:03

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 03/03/2019