Swali: Je, inajuzu kutumia dalili kwa kauli miongoni mwa kauli za wanachuoni ya kwamba adhaana ya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) ya Ijumaa baada ya zama za Maswahabah inahesabika ni Bid´ah?

Jibu: Huyu sio mwanachuoni mwenye kusema kuwa adhaana ya kwanza ambayo aliamrisha ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye ndio khaliyfah wa tatu miongoni mwa makhaliyfah waongofu, kuwa ni Bid´ah. Aliiamrisha katika zama za Muhaajiruun na Answaa pia na hawakumkataza. Huyu sio mwanachuoni juu ya masuala haya. Hata kama anaweza kuwa mwanachuoni katika mambo mengine pamoja na hivyo ni mjinga katika masuala haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14759
  • Imechapishwa: 28/06/2020