Mwenye kumwambia “Mke wake wewe ni haramu kwangu ukifanya kadhaa”


Swali: Kuna mtu kamwambia mke wake: “Wewe utakuwa ni Haramu kwangu ukienda kwenye nyumba ya kaka yako.” Ipi hukumu ya hilo na khaswa ikiwa karejesha kauli yake na kumsamehe mke wake amtembelee kaka yake?

Jibu: Hii ni Dhwihaar. Analazimika kutoa kafara ya Dhwihaar. Na wala asimsogelee mke wake mpaka atoe kafara ya Dhwihaar. Nayo ni kuacha mtumwa huru ambaye ni muumini, akikosa afunge miezi miwili mfululizo, ikiwa hawezi alishe masikini sitini. Kujiharamishia mke ni Dhwihaar.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/2924
  • Imechapishwa: 18/02/2018