Mwenye kujiua atadumishwa Motoni milele?

Swali: Ni ipi hukumu ya muislamu ambaye anajiua? Je, atadumishwa Motoni milele?

Jibu: Mwenye kuiua nafsi yake amefanya dhambi kubwa. Ni kama mfano wa mtu ambaye amemuua mwengine. Nafsi yako sio milki yako. Yule mwenye kuiua nafsi yake au akamuua mwengine juu yake yako matishio makali. Imepokelewa katika Hadiyth:

“Mwenye kuia nafsi yake kwa kitu basi ataadhibiwa kwacho siku ya Qiyaamah.”

Haya ni matishio. Hakufuru isipokuwa akiona kuwa kitendo hicho ni halali. Akihalalisha kumuua muislamu au akahalalisha kumuua muislamu anakufuru. Lakini midhali hahalalalishi kitendo hicho ni mtenda dhambi kubwa. Hivyo yuko chini ya matakwa ya Allaah.

Akiwa na ugonjwa wa akili ambaye ´ibaadah hazimuwajibikii akiiua nafsi yake ni mwenye kupewa udhuru. Lakini ni lazima kwa msimamizi wake amchunge, asimpuuze na wala asimwache na kitu ambacho anaweza kujiua kwacho nafsi yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191634
  • Imechapishwa: 11/04/2020