Swali: Kwa mfano mwenye kusema ya kwamba yule anayesujudia sanamu hahesabiki kuwa ni kafiri mpaka aamini [kujuzu kwa] hilo ndani ya moyo wake. Je, maneno yake ni sahihi?

Jibu: Haya ni maneno ya Murji-ah. Mwenye kufanya kufuru ni kafiri. Isipokuwa ikiwa kama atakuwa kafiri na apewe udhuru kwa ujinga. Ama ikiwa ana elimu na ni mjuzi, pale anapofanya kufuru anakufuru. Mwenye kusujudia sanamu anakufuru. Mwenye kuchinja kwa asiyekuwa Allaah anakufuru. Mwenye kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah anakufuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_14.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2018