Swali: Je, mwenye kufanya Bid´ah anakufuru kwa sababu anaweza kuamini kuwa uongofu wake ni mkamilifu zaidi kuliko wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Akiamini imani hii anakufuru. Lakini wengi wao hawana imani hii. Lakini huona kuwa ni Bid´ah nzuri na kwamba inamkurubisha mtu kwa Allaah. Hawaonelei kuwa alichokifanya ni bora kuliko Sunnah. Ama akiamini hivo anakufuru pasi na shaka. Lakini anachodai ni kwamba kitu hichi ni kizuri, kinamkurubisha kwa Allaah, ndani yake kuna malipo n.k.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
  • Imechapishwa: 17/11/2018