Mwenye hedhi kusoma Qur-aan katika simu


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kusoma Qur-aan kwenye simu?

Jibu: Hapana, mwenye hedhi hasomi Qur-aan. Isipokuwa wakati wa haja. Akikhofia kuwa atasahau Qur-aan anaweza kusoma ili iweze kubaki kichwani mwake. Kadhalika akikhofia asije kufeli katika mtihani anaweza kusoma kwa haja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13965
  • Imechapishwa: 13/04/2018