Nimepata kigezo kizuri kabisa juu ya ni nani anayestahiki kuitwa “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah”. Kidhibiti hichi kimeandikwa na imamu miongoni mwa maimamu wa Sunnah na mwanaume bingwa, mtu aliyepambana na Ahl-ul-Bid´ah: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin ´Aliy al-Barbahaariy. Kidhibiti hichi amekitaja kwenye kitabu chake “Sharh-us-Sunnah” ifuatavyo:

“Haijuzu kwa yeyote muislamu kusema kuwa mtu fulani anafuata Sunnah mpaka ajue kuwa amekusanya sifa zote za Sunnah. Hakusemwi kuwa ni mtu anayefuata Sunnah mpaka zikusanyike kwake sifa za Sunnah zote.”[1]

Mtu aliye namna hii ndiye anayestahiki kuitwa “Ahl-us-Sunnah”.

Hivyo ambaye anasema kuwa Ashaa´irah ni katika Ahl-us-Sunnah amesema uongo na kuzua. Amche Allaah (Ta´ala). Ambaye anataka kusema kuwa mtu fulani ni katika Ahl-us-Sunnah basi ni lazima kwanza ajue kuwa mtu huyu anafuata Sunnah na Ahl-us-Sunnah. Hakika zama hizi ni zama za fitina juu ya dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Ni watu wangapi ambao udhahiri wao ni Sunnah, lakini ukipeleleza uhalisia wake utaona namna anavyoikataa Sunnah katika mambo mengi!

Kwa hivyo ni lazima kuwa makini na kuthibitisha kwanza. Ni kama alivyofanya Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anh) pindi alipochukua majiwe mawili na akaliweka limoja juu ya lingine kisha akawaambia marafiki zake:

“Hivi mnaona mwanga wowote kati ya majiwe haya mawili?” Wakasema: “Ee Abu ´Abdillaah! Hakika hatuoni mwanga isipokuwa mdogo sana.” Hudhayfah akasema: “Ninaapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake Bid´ah zinadhihiri mpaka haki itaonekana kama mwanga ulio kati ya mawe haya mawili. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba Bid´ah itaenea kiasi cha kwamba atayeacha Bid´ah atakuja kutuhumiwa kuwa ameacha Sunnah.”[2]

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba maneno yake (Radhiya Allaahu ´anh) yanaenda sambamba kabisa na zama zetu hizi. Allaah atukinge sisi na nyinyi dhidi ya kila baya.

[1] Sharh-us-Sunnah (57).

[2] al-I´tiswaam (1/127) ya ash-Shaatwibiy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 40-42
  • Imechapishwa: 09/08/2020