Mwanaume kuvaa Hijaab kwa ajili ya mzaha

Swali: Je, ni haramu kwa mwanaume kujifananisha na wanawake ilihali anafanya mzaha kama kwa mfano mwanaume akavaa Hijaab kwa lengo la kuwachekesha marafiki zake?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake na wanawake wenye kujifananisha na wanaume. Ni mamoja ikiwa ni kwa kufanya mzaha au kutofanya mzaha. Haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2120
  • Imechapishwa: 09/07/2020