Mwanaume kufunika uso wakati wa Ihraam

Swali: Inafaa kwa mwanaume Muhrim kufunika uso wake wakati wa kulala?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo japokuwa wanachuoni wametofautiana. Lakini maoni sahihi ni kwamba hakuna neno. Kilichokatazwa ni kufunika kichwa chake. Ama kufunika uso hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (22) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-26-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 22/03/2020