Swali 903: Kuna mwanamke ambaye ameolewa na mwanaume ambaye anapoingia nyumbani basi huwapiga watoto wake na mke wake. Tunaomba umnasihi mtu huyu na mfano wake?

Jibu: Mwanaume huyu ni mwenye kumuasi amri ya Allaah na anakhalifu Shari´ah Yake. Kwa sababu Allaah (Subhaanah) amewaamrisha waume kuishi na wake kwa wema. Si katika wema mwanaume kuingia nyumbani mwake hali ya kuwa ni mwenye ghadhabu, akikemea, akikaripia na akipiga. Hakuna anayefanya hivi isipokuwa mtu ambaye ni mwenye akili na dini pungufu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 361
  • Imechapishwa: 15/09/2019