Mwanamume ndiye mwenye kumtawala mwanamke katika Biblia

16Kisha akamwambia mwanamke:

“Nitakuzidishia uchungu wa kuzaa,

kwa uchungu utazaa watoto.

Hata hivyo utakuwa na hamu na mumeo,

naye atakutawala.”

17Kisha akamwambia huyo mwanamume:

“Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo,

ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile,

kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa.

Kwa jasho utajipatia humo riziki yako,

siku zote za maisha yako.

18Ardhi itakuzalia michongoma na magugu,

nawe itakubidi kula majani ya shambani.

19Kwa jasho lako utajipatia chakula

mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa,

maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.”

20Adamu akampa mkewe jina “Hawa”, kwa sababu alikuwa mama wa binadamu wote. 21Mwenyezi Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mwanzo 03:16
  • Imechapishwa: 15/01/2020