Swali:  Allaah (Ta´ala) amesema:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao. Basi wanawake wema watiifu, wenye kuhifadhi hata wanapokuwa hawapo [waume zao] kwa kuwa Allaah [ameamrisha] wayahifadhi. Na wale [wanawake] ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na [wakiendelea uasi] wahameni katika vitanda na wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia. Hakika Allaah yuko juu kabisa na Ametukuka.” (04:34)

Ni ipi tafsiri ya Aayah hii? Ni nini maana ya “uasi”?

Jibu: Maana yake ni kwamba mwanaume ndiye msimamizi wa mwanamke, kumhudumikia, kumtengea makazi, kumlinda, kumhifadhi na upindaji. Yeye ndiye mwenye kumchunga, ataulizwa juu yake siku ya Qiyaamah. Asimwache akaingia na kutoka apendavyo. Yeye ndiye msimamizi wake.

Swali: Nini maana ya uasi?

Jibu: Ni mke kumuasi mume. Uasi ni yeye [mwanamke] asimpe haki yake ya kitandani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=9b7Lve_g1Q0
  • Imechapishwa: 19/05/2018