Mwanamume Kufuga Nywele


Swali: Kuachia nywele ndefu ni katika Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Imependekezwa endapo ataziachia katika ile sifa yenye kuafikiana na nywele za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo haijuzu ikiwa ataziachia kama wanavyofanya makafiri au watu wanaofanana nao.

Isitoshe anatakiwa kufuata desturi ya pale anapoeshi. Ikiwa watu wa mji wanaacha nywele kwa njia ya Sunnah, naye aziache nywele zake. Vinginevyo asifanye hivo. Katika hali hii itakuwa ni kutaka kuonekana kati ya watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kutaka kuonekana na mavazi ya kutaka kuonekana (Shuhrah). Hii ni Sunnah, sio wajibu wala lazima. Ikiwa hilo linaleta lawama au ni geni hapo anapoeshi, aachane na kitu hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017