Mwanamke wa Sunnah haolewi na mwanaume wa Bid´ah


Swali: Kuna mwanamke ni katika Ahl-us-Sunnah. Anataka kuolewa na mwanaume ambaye yuko na Bid´ah. Mwanamke huyo hafanyi hizo Bid´ah zake ila anasema kuwa huenda akakubali haki. Je, anaweza kuolewa naye na ni ipi hukumu ya kuhudhuria ndoa hii?

Jibu: Mtu anayeitendea kazi Sunnah haolewi na mtu wa Bid´ah. Kwa kuwa atamuathiri yeye na watoto wake. Isipokuwa ikiwa kama atatubu. Akitubu kabla ya ndoa na akaacha Bid´ah, Tawbah ambayo ni ya kweli kabisa, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mntq--14340427.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2020