Mwanamke Wa Kirusi Anakusanya Swalah Zote Jioni Anapotoka Kazini

Swali: Mwanamke aliyetoka karibuni kusilimu kutoka Urusi anasema kuwa anafanya kazi kati ya makafiri na anakusanya swalah zote jioni. Ni ipi hukumu ya kukusanya kwake swalah zake?

Jibu: Haijuzu. Swalah inatakiwa kuswaliwa kwa wakati wake. Swali swalah kwa wakati wake. Haijuzu kwake kufanya hivi. Mwanamke kama huyu wa Kiislamu haijuzu pia kwake kufanya kazi na makafiri. Atafatute kazi nyingine:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote anayemcha Allaah; basi atamjaalia njia ya kutoka na atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.” (65:02-03)

Afanye kazi na waislamu wenzake katika nchi yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 01/11/2016