Swali: Ipi hukumu ya vipodozi maquillage kwa mwanamke?

Jibu: Imethibiti ya kwamba ina madhara kama nilivyoona mwenyewe katika maandiko ya kwamba inamdhuru mwanamke. Na huenda ikazeekesha uso wake mapema. Ni Haramu hata kama itakuwa haina madhara. Na ni kijifananisha na maadui wa Uislamu. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Yule mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.”

Na mimi, bali hata nyie mnaamini kuwa mambo haya yalikuwa hayajulikani mpaka yalipotujia kutoka kwa maadui wa Uislamu na tukajifananisha na maadui wa Uislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/Default_ar.aspx?id=6022
  • Imechapishwa: 18/02/2018