Mwanamke si katika mali zenye kurithiwa

Swali 770: Ni ipi hukumu ya kumzingatia mwanamke ni miongoni mwa vyenye kurithiwa nyumbani kwa mume?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemharamisha mwanamke kuwa miongoni mwa vyenye kurithiwa. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا

“Enyi walioamini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa kuwakirihisha.”[1]

Amedhamini utuwake kuwa kipekee na akamfanya kuwa ni mrithi na si mwenye kurithiwa.

[1] 04:19

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 301
  • Imechapishwa: 04/08/2019