26 Nami nilikuwa nikivumbua:

Jambo lenye maumivu zaidi ya kifo,

nikampata mwanamke ambaye yeye mwenyewe ni nyavu za kuwinda

na moyo wake ni nyavu za kukokota na ambaye mikono yake ni pingu.

Mtu ni mwema mbele za macho ya Mungu wa kweli ikiwa anaponyoka kutoka kwake,

lakini mtu anafanya dhambi ikiwa ananaswa naye.

27Tazama! nimevumbua hili:

Akasema mkutanishaji,

Kitu kimoja kikichukuliwa baada ya kingine ili kujua jumla yake,

28ambayo nafsi yangu imetafuta kwa kuendelea, wala sijaiona. Nimemuona mwanamume mmoja kati ya elfu moja,

lakini sijamwona mwanamke mmoja kati yao wote.

29Tazama! Nimeona hili peke yake:

Ya kwamba Mungu wa kweli aliwafanya wanadamu wakiwa wanyoofu,

lakini wao wenyewe wametafuta mipango mingi.”

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mhuburi 07:26
  • Imechapishwa: 17/01/2020