Mwanamke mwolewaji anataka kurudi kwa yule mume wa kwanza


Swali: Mwanaume akitaka kumuoa mwanamke na akawa amefanya hivo. Kisha baadaye akaja kujua kuwa mwanamke anataka kurudi kwa yule mume wake wa kwanza ambapo akamtaliki juu ya hilo. Je, inajuzu kwake kurudi?

Jibu: Amemtaliki kwa kutaka kwake mwenyewe. Kizuizi kiko wapi cha kurudi kwa yule mume wake wa kwanza wakaoana kwa kufunga ndoa mpya? Hakulazimishwa kumtaliki. Amemtaliki kwa kutaka kwake mwenyewe baada ya kutomtaka tena.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 27/10/2017