Mwanamke mwenye nifasi kufunga kabla ya kutimia siku 40

Swali: Ikiwa mwanamke damu yake ya nifasi imekatika kabla ya kutimia siku 40 baada ya kuzaa. Je, swawm yake ni sahihi?

Jibu: Swawm yake ni sahihi kwa kuwa imesafika damu yake. Sawa bila ya kujali kumepita chini ya siku 40 kwa sababu [ikikatika damu yake] anafuata hukumu moja kama ya wanawake wengine wote ambao wako Twahara na damu ya uke.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan as-Sa’diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa ad-Sa’diyyah uk, 138
  • Imechapishwa: 24/09/2020