Mwanamke mwenye hedhi na nifasi kushika msahafu na kuingia msikitini


Swali: Ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi kugusa msahafu pasina kizuizi? Na ni ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi na nifasi kuingia Msikitini?

Jibu: Kugusa msahafu pasina kizuizi ni kwamba inajuzu kwa kukosekana dalili sahihi zinazopinga hilo. Ama Kauli Yake (Ta´ala):

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ

“Hawaigusi isipokuwa waliotwahara.” (56:79)

makusudio hapa ni Malaika. Kama Alivyosema hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Kitabu Chake Kitukufu:

  وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ

“Na (wala) hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan. Na (wala) haipasi kwao (kuteremka na Qur-aan) na wala hawawezi.” (26:210)

“Iliyoifasiri Aayah hii vizuri, ni Kauli nyingine ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ بِأَيْدِي سَفَرَةٍ كِرَامٍ بَرَرَةٍ

“Sivyo katu! Hakika (hizi Aayah za Qur-aan) ni ukumbusho. Basi atakaye akumbuke. (Zimeandikwa) Katika swahifa zilizokirimiwa (Al-Lawh Al-Mahfuwdh). Zimetukuzwa na zimetwaharishwa. (Zinazobebwa) Katika mikono ya (Malaika) waandishi. Watukufu (na) watiifu.” (80:11-16)

Na makusudio hapa katika Aayah hii ni Malaika. Hivyo Aayah hii ya al-Waaqi´ah makusudio ni Malaika. Na Allaah (Ta´ala) ndiye Mwenye Kujua zaidi. Ama mwanamke mwenye hedhi na nifasi kuingia Msikitini, sijui kama kuna dalili yoyote katika Kitabu na Sunnah inayokataza hilo. Ama kuhusu Hadiyth:

“Mimi sikuhalalisha Msikiti kwa aliye na hedhi na janaba.”Hadiyth hii ni dhaifu. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamwambia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha):

“Hedhi yako haiko mikononi mwako.”

Na alimwambia tena (´alayhis-Salaam):

“Hapana! Fanya anayopasa kufanya mwenye kuhiji, isipokuwa tu usitukufu kwenye Ka´abah.”

Na katika zama za Mtume kulikowepo mwanamke ambaye anafanya kazi Msikitini na anaishi Msikitini. Na mwanamke huyu alikuwa kishakuwa mama, anajiwa na yanayowajia wanawake wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi katu kumwambia:

“Unapojiwa na hedhi, toke nje (ya Msikiti).”

Hapa kuna dalili inaonesha kuwa, inajuzu kwa mwanamke kuingia Msikitini naye yuko na hedhi au nifasi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=284
  • Imechapishwa: 18/02/2018