Mwanamke mtalikiwa anamtaka mume wake wa kwanza baada ya talaka tatu


Swali: Mwanaume akienda kumposa mwanamke mtalikiwa ilihali anajua kuwa huyu mwanamke hamtaki na atafanya bidii zote amtaliki ili aweze kurudi kwa yule mume wa kwanza. Je, katika hali hii itafaa kwa mwanaume huyu kwenda kumposa?

Jibu: Hapana, haijuzu kwake kufanya hivo. Asende ilihali anajua kuwa hampendi na badala yake anampenda yule mume wake wa kwanza. Anachotaka mwanamke huyu ni kumfanya mwanaume huyu kama njia ya kumwendea yule mume wa kwanza. Haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017