Swali: Kuna mwanamke alikuwa na hedhi na ilipofika usiku akaona alama ya kutwaharika. Hivyo akawa ameoga na kufunga siku ya pili. Wakati wa mchana akatokwa na kitu kidogo katika damu pamoja na kujua ya kwamba ametoka katika siku zake ambazo amezoea kupata hedhi kila siku. Je, afunge na kuswali au hiyo ni damu ya hedhi? Ni ipi hukumu ikiwa damu hii ndogo itaendelea kwa masiku?

Jibu: Mwanamke huyu akiwa na uhakika wa kutwaharika mwishoni mwa usiku na akafunga, tone moja mbili baada ya kutwahirika si lolote. Haimzuii swalah wala swawm. Ni kama mfano wa umanjano na uchafuchafu. Swawm ya mwanamke huyu ni sahihi na hatoilipa. Hata kama itakuja katika siku ya pili, tatu na nne tone moja mbili si kitu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 23/09/2020