Mwanamke kuweka sharti kuolewa na mtafutaji elimu


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuweka sharti kwa anayemchumbia awe mtafutaji elimu [ya Kishari´ah]?

Jibu: Swali haliko wazi vizuri. Yaani kaweka sharti kwa anayemchumbia awe katika wanafunzi. Kwa hiyo nini tatizo? Anataka mwanaume awe mwema, vizuri anataka pia awe na kazi nzuri – mwema na mtafuta elimu. Kwa hiyo atapoweka sharti hii ya kuwa awe mtafutaji elimu, lakini yaani haimaanishi kuwa atakuwa mwema. Kwa hiyo anamaanisha [atayemchumbia] awe mwema na mtafutaji elimu. Nini tatizo ya hili? Ingelikuwa wanawake wote wako aina hii.

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ

“Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa waoni marafiki walinzi.”

يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَـئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللّهُ إِنَّ اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

“Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika swalah na hutoa zakaah na humtii Allaah na Mtume wake. Hao Allaah atawarehemu. Hakika Allaah ni Mtukufu Mwenye nguvu asiyeshindika, Mwenye hikima.” (09:71)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/LNNMJTFlX-4
  • Imechapishwa: 17/09/2020