Swali: Baadhi ya wanawake wanapokuwa masomoni au nchikavu wanaswali na kuweka ´Abaa´ah zao juu ya mabega yao. Je, kitendo hichi kinajuzu?

Jibu: Hakuna neno. Kuna nini katika kufanya hivo? Mwanamke tokea hapo kitambo anaposwali anaweka ´Abaa´ah juu ya mabega yake[1]. Huku hakuzingatiwi ni kujifananisha na wanaume. Hili ndio vazi la wanawake. Kujifananisha kunakuwa katika kitu ambacho amepwekeka nacho ile jinsia nyingine na wala hiyo jinsia nyingine haikifanyi. Ama ikiwa ni kitu ambacho kinatambulika kati ya pande zote mbili, huku sio kujifananisha. Sioni ubaya juu ya hili.

Jengine ni kwamba namna ilivyo shungu ya mwanamke sio kama kilivyo kilemba cha mwanaume. Hiki ni kivazi kisichofanana na kivazi cha mwanamke kwa njia zote. Sio ubaya kufanya hivo – Allaah akitaka.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/mwanamke-kuweka-abaaah-juu-ya-mabega-wakati-kuswali/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/909
  • Imechapishwa: 08/09/2018