Mwanamke kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega wakati wa kuswali


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega wakati wa swalah?

Jibu: Ndio, hakuna neno. Kufanya hivi kunaweza kuwa kunamlinda na ni kwepesi zaidi kwake kuliko ibaki kila pale ´Abaa´ah inamtoka kichwani mwake anairudisha tena. Huku sio kujifananisha na wanaume. Muonekana wa mwanamke katika hali hii haifanani na muonekana wa wanaume.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/787
  • Imechapishwa: 20/01/2018