Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuvaa shati la kike na suruwali ya kike lakini suruwali hii ni pana ya kuachia na si ya kubana? Ni ipi hukumu ya kuivaa na kuwavalisha wasichana wadogo?

Jibu: Inazingatiwa ni kujifananisha na maadui wa Uislamu. Tunawashauri kujiepusha nayo. Vivyo hivyo wasichana wadogo watazowea hilo na kuendelea kufanya hivyo watapokuwa wakubwa. Tunawashauri kushikamana na dini ya Uislamu na sisi, wasichana wetu na familia zetu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3794
  • Imechapishwa: 07/09/2020