Swali: Hadiyth ambayo imependekeza kuvaa mavazi meupe, je, ni kwa wanaume na wanawake? Na je, ni jambo lililopendekezwa hata kwa wanaume?

Jibu: Lilio la dhahiri ni kuwa ni kwa wanaume. Kwa dalili ya Hadiyth ya ´Aaishah, ya kwamba aliona wanawake wa Answaar wametoka kwa ajili ya Swalah ya Fajr na walikuwa wamevaa mavazi meusi. Pamoja na haya, sio Haramu kwa mwanamke kuvaa mavazi meupe. Jambo lililo la Haramu kwake ni kujifananisha na wanaume. Kama ilivyokuja katika Swahiyh:

“Allaah Anamlaani mwanaume anayejifananisha na mwanamke; na mwanamke anayejifananisha na mwanaume.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=650
  • Imechapishwa: 20/02/2018