Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke anayetoka nyumbani kwake kwenda masomoni ilihali hakujitia manukato lakini pale tu anapoingia masomoni basi anaweka manukato na mwanamke huyo anakaa kwenye masomo yake karibu masaa manne?

Jibu: Hakuna kizuizi. Hakuna neno akijitia manukato na yeye yuko kati ya wanawake tu. Vivyo hivyo wakati wa kutoka ikiwa anatoka pamoja na Mahram yake haidhuru pia. Lakini akiwa anatoka pamoja na dereva wa kiume ambaye si Mahram yake basi anatakiwa kutumia manukato yenye rangi lakini yasiyokuwa na harufu. Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba manukato ya mwanamke ni yale yasiyokuwa na harufu, ingawa katika cheni ya wapokezi wake kuna udhaifu. Lakini mwanamke anatakiwa kulizingatia jambo hilo. Usitumie manukato katika vijia wala pamoja na dereva wa kando. Jambo ni lenye wasaa akiwa anaitumia masomoni tu manukato yasiyokuwa na harufu kali ili harufu yake iweze kuondoka wakati wa kuondoka kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4415/حكم-وضع-الطيب-للمراة-بحضرة-النساء
  • Imechapishwa: 06/06/2020