Mwanamke kutumia dawa za kuharakisha hedhi ili atoke ndani ya eda

Swali: Ni haki kwa mwanamke mtalikiwa ambaye anapata hedhi kila baada ya miezi miwili kutumia dawa za kuteremsha hedhi ili isirefuke eda yake?

Jibu: Asifanye hivo. Kwa sababu mume wake ana haki. Pengine pamoja na kurefuka muda wa eda mume akamrejea. Mke akirejelewa na mume wake ndani ya eda, basi ana haki ya kufanya hivo bila ya mahari wala kufunga ndoa upya. Kwa hivyo kule kuharakisha kwake hedhi ili eda iweze kwisha, kitendo hichi kina madhara kwa mume na kuangusha haki yake. Asifanye hivo. Tukikadiria kuwa mume wake hana tena haki ya kumrejea kama kwa mfano anakaa eda ya talaka ya mwisho, kunaweza kusemwa kwamba hakuna neno akatumia dawa za kuharakisha hedhi ili astarehe kutoka katika eda na aolewe na mwanaume mwingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1254
  • Imechapishwa: 27/09/2019