Mwanamke kutoa darsa kwa njia ya intaneti


Swali: Ipi hukumu kwa mwanamke kutoa muhadhara kwenye intaneti wakisikia sauti yake wanaume?

Jibu: Mwanamke hana haja ya kuwatolea muhadhara watu wote, wanaume na wanawake. Ni mamoja kwa njia ya intaneti au njia zingine. Mwanamke hana haja ya hilo. Kuko wanaoshughulikia kazi hii ya mihadhara pasina kuwa mwanamke. Mwanamke inatosheleza kwake kufunza katika jamii yake, jirani zake, katika mujtamaa ambapo yeye anaeshi ikiwa kutaaminika fitina, afunze. Wala haijuzu kwa mwanamke kutafuta kheri kwa mambo ambayo yatamsababishia kupata madhambi akaja kuadhibiwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.njza.net/Default_ar.aspx?ID=98
  • Imechapishwa: 15/09/2020