Swali: Mwanamke akifika al-Madiynah amekuja kufanya Hajj au ´Umrah inafaa kwake kwenda kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au hapana?

Jibu: Haifai kwake kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna udharurah wa yeye kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtu anapomswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kokote pale atapokuwepo – basi salamu zake zinamfikia. Hivyo basi, hakuna udharurah wowote wa yeye kusimama mbele ya kaburi lake na kumtolea salamu.

Isitoshe wanachuoni wengi wanasema mwanamke akitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaingia katika laana. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Kwa hivyo asilitembelee kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inatosha kwake kumswalia akiwa ndani ya msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nyumbani kwake au kokote pale.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (34) http://binothaimeen.net/content/751
  • Imechapishwa: 26/11/2017