Swali: Bora kwa mwanamke ni kuswali hali ya kuwa amefunua uso wake au ameufunika wakati kunapokuwa hakuna wanaume wasiokuwa Mahram zake? Kufunika paji lake la uso kumechukizwa wakati wa Sujuud?

Jibu: Bora kwa mwanamke wakati anaposwali afunue uso wake ikiwa mbele yake hakuna wanaume mbali na Mahram. Kwa kuwa hilo ni bora wakati wa swalah na viungo vya mwili vitaweza kugusa katika ardhi. Ama kukiwa wanaume ajinabi ni wajibu kwake kufunika. Wakati wa Sujuud bora ni paji la uso liguse sehemu ya kusujudia. Kutokana na hili, wakati anapotaka kusujudu, hata kama kutakuwa wanaume, afunue uso wake ili uso uweze kugusa katika ardhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 01
  • Imechapishwa: 23/09/2020