Mwanamke kuswali msikitini pasina idhini ya mume

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuswali msikitini hali ya kuwa amejisitiri, amejiheshimu, hakujitia manukato na wala haonyeshi manukato na yeye amefanya hivo kwa kutaka uso wa Allaah mbali na kwamba mume wake haridhii jambo hilo?

Jibu: Inafaa kwa mwanamke kuswali msikitini akiwa amejisitiri na hakujitia manukato. Haifai kwa mumewe kumzuia kutokamana na hilo akilazimiana na zile adabu za ki-Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah.”[1]

“Mmoja wenu akiombwa idhini na mke wake ya kwenda msikitini basi asimkatalie.”[2]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Akitoka nje kwa staha na pasi na manukato hapana neno ijapo mume wake si mwenye kuridhia kutokana na Hadiyth mbili zilizotajwa. Na akiswali nyumbani kwake na asitoke kwa sababu ya kuitakasa nafsi yake na kujiepusha na sababu za fitina ndio bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah na nyumba zao ni bora kwao.”[3]

[1] al-Bukhaariy (849) na Muslim (668) na tamko ni lake.

[2] Ahmad (4328), al-Bukhaariy (4837) na Muslim (666).

[3] Ahmad (5211) na Abu Daawuud (480).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/79)
  • Imechapishwa: 20/11/2021