Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kutoka mji kwenda mwingine akiwa pamoja na mtoto wa kiume wa dada yake kwa ajili ya matibabu naye (mtoto huyo) hajafikisha umri wa kuota ?

Jibu: Ikiwa mtoto huyo anaweza kupambanua mambo, hakuna ubaya kwa hili. Na aghlabu ambaye kishafikisha miaka 10, 11 au 13 anakuwa ni mwenye kuweza kupambanua. Hakuna ubaya kusafiri pamoja naye ikiwa kutaaminika fitina. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Sio Halali kwa mwanamke ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1062
  • Imechapishwa: 20/02/2018