Swali: Mimi ninawasalimia na mkono watoto wa shangazi yangu na mjomba wangu bila ya kizuizi. Je, hili linajuzu? Na ikiwa haijuzu, je naweza kuweka mkononi mwangu abaya na vifuniko vya mikono (gloves)?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kupeana mikono na wanaume ikiwa sio Mahaarim zake; kama mfano wa watoto wa shangazi na mjomba wake, hakika hawa sio Mahram zake. Haifai kwake kupeana nao mikono, sawa ikiwa kwa kuweka kizuizi au bila ya kuzuizi. Isipokuwa anaweza kupeana mikono na Mahaarim zake; kama kwa mfano wa kaka yake, mjomba wake, shangazi yake, baba yake au wanawake wenzake haina neno. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mimi sipeani mikono na wanawake.”

Mwanaume asipeani mokono na mwanamke, na mwanamke asipeani mikono na mwanaume ambaye sio Mahram wake; kama kwa mfano wa mtoto wa shangazi yake, mjomba wake, jirani yake, mume wa dada yake, kaka wa mke wake. Wote hawa ni watu ajinabi kwake, haifai kwake kupeana nao mikono, sawa iwe kwa kuweka kizuizi au pasina kizuizi

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 16/03/2018