Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuonesha sehemu katika nywele zake kwa kukusudia pamoja na kuvaa ´Abaa´ah na shungi? Je, kwa kufanya hivi anazingatiwa kuwa ni mwenye kufanya mapungufu katika Hijaab au ni mwenye kuonesha mapambo?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kuonesha kitu katika nywele zake. Bila ya shaka huku ni kuonesha mapambo yake. Ni wajibu kwake kuficha nywele zake, mikono yake na miguu yake. Mwili wa mwanamke wote ni ´Awrah.
Lakini hata hivyo ikiwa ni katika Swalah aoneshe uso wake ikiwa hakuna wanaume ajinabi. Ikiwa kuna wanaume ajibali afunike uso wake hata wakati wa Swalah.

Miongoni mwa mambo ambayo baadhi ya wanawake wanayachukulia usahali ni kufunika nyuso zao lakini wakati huo huo wanaonesha mikono yao na kuiacha wazi ambapo kunaonekana pete alizovaa na vinginevyo. Mikono yake ni ´Awrah. Ni wajibu kwake kufunika mikono yake kwa nguo yake au ´Abaa´ah yake au vifuniko vya mikono.

Hakuna tofauti juu ya kwamba mikono ni ´Awrah. Hata wale ambao wanasema kuwa mwanamke kufunika uso wake sio wajibu wanasema vilevile kuwa ni wajibu kwake kufunika mikono yake na miguu yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.islamway.net/lesson/138827/%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A3%D8%A9-%D8%AD%D9%82%D9%88%D9%82-%D9%88%D9%88%D8%A7%D8%AC%D8%A8%D8%A7%D8%AA?ref=s-pop
  • Imechapishwa: 24/09/2020