Mwanamke kuondosha nywele za kwenye kidevu, miguuni na mwilini


Swali: Je, inajuzu kuondosha nywele zilizo kwenye mwili wa mwanamke au miguuni mwake?

Jibu: Ama kama ni kujuzu, inajuzu. Ama kukipatikana dawa akaziondosha mara moja, ni sawa. Ama nywele ambazo ziko miguuni mwa mwanamke sio mbaya. Lakini nywele za kwenye kidevu, hakuna ubaya akaziondosha au akatumia dawa ambayo itafanya zisijitokeze mara nyingine. Na kama sikukosea nadhani ni an-Nawawiy ambaye amesema kuwa ni wajibu kwa mwanamke kuondosha nywele za kwenye kidevu ili asijifananishe na mwanaume. Ama nywele za kwenye miguu yake, hakuna ubaya akaziondosha na si kama ndevu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1067
  • Imechapishwa: 22/02/2018