Mwanamke kuondosha nywele usoni mwake

Swali: Ni ipi hukumu ya kuonodosha nywele zinazoota kwenye uso wa mwanamke?

Jibu: Ni jambo linahitajia upambanuzi. Ikiwa ni nywele za kawaida basi haijuzu kuziondosha kutokana na Hadiyth:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke mwenye kuchonga nyusi na mwenye kuchongwa, mwanamke mwenye kutengeneza mwanya na mwenye kutengenezwa na wanamke mwenye kuunganisha nywele na mwenye kuunganishwa.” [1]

Namsw (النمص) ni kule kuondosha nywele usoni kukiwemo nyusi. Lakini ikiwa ni nywele nyingi zinazomuumbua, kama mfano wa masharubu na ndevu, basi hakuna neno wala ubaya kuziondosha. Kwa sababu zinamuumbua na kumdhuru.

[1] al-Bukhariy (5941).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1985/ازالة-الشعر-النابت-في-وجه-المراة
  • Imechapishwa: 19/03/2021