Mwanamke kuomba talaka kwa mume ambaye ni tasa


Swali: Kuna mwanamke ameolewa miaka saba iliyopita na ripoti za kidaktari zimethibitisha kuwa mume wake hana uzazi. Je, anaweza kumuomba talaka mume wake huyu ambaye hana uzazi? Unamnasihi nini?

Jibu: Ndio, inafaa kwake kuomba talaka. Kwa sababu ana haki ya kupata watoto. Ikithibiti kuwa kweli mume wake ni tasa, basi ana haki ya kufuta talaka. Lakini kunabaki kitu kimoja; je, lililo bora ni yeye kuomba kufutwa kwa ndoa au bora ni yeye kubaki pamoja naye? Anatakiwa kutazama. Ikiwa mwanamume huyu ni mtu wa kheri, wa dini na wa tabia, basi ni sawa akabaki pamoja naye. Vinginevyo lililo bora ni yeye kutafuta mume ambaye anaweza kupata naye watoto. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Oeni wanawake wenye kuzaa sana na wenye mahaba.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/827
  • Imechapishwa: 14/03/2018