Mwanamke kuolewa na mwanaume Salafiy


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke akimpata mwanaume mwenye msimamo katika manhaj ya Salaf-us-Swaalih kuiwasilisha nafsi yake kwake kwa ajili ya ndoa, na ipi nasaha yako?

Jibu: Kwa hakika, kutafuta mwanaume mzuri ni jambo ambalo Shari´ah yalisisitiza, kwa kuwa maisha ya ndoa yana umuhimu na athari yake, kutafuta kwake mwanamke mwanaume mwema ni dalili ya wema wake. Mwanamke huyu, kama kuna uwezekano maneno yakawa baina ya walii wake na baina ya huyo anayetaka kumchumbia hili ni bora. Atamwachia jambo hili msimamizi wake. Na ikiwa hawezi kuongea na msimamizi wake, atamtumia dada yake mkubwa kama mama au dada na mfano wa hao, kisha anaweza kuwakilisha qadhiya hii na lengo la ndoa ili asije kumkosa mwanaume mzuri. Hili halina makosa.

Ama ikiwa makusudio ya yeye kujiwasilisha, ni mazungumzo, au kwa uhusiano ambao unajulikana hivi leo, kama kuoneshana mapicha, kupeana mapicha, na kupigiana masimu; hili madhara yake yako wazi kwa watu. Muhimu ni kuwa, ombi lake ni zuri lakini inatakiwa iwe kwa sura nzuri na ya heshima. Si kwa maana ambayo imezoeleka leo kama kwa intanet na simu n.k. Ikiwa itatokea kuongea nae kwa njia ya simu lengo lake la ndoa, hivyo inatakiwa iwe neno moja tu. Nako ni kuwakilisha ombi la ndoa na inatosha hivo. Ama kukalia mazungumzo, hili halijuzu mpaka hapo atapokuwa mke wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/1LFJ8HjGHsg
  • Imechapishwa: 19/09/2020