Mwanamke kumvalia mume wake suruwali nyumbani


Swali: Mbele ya mume wake nyumbani kwake, [ikiwa atavaa suruwali] kama vazi la usiku [akilala nalo] na mfano wa hilo?

Jibu: Mbele ya mume asivae suruwali kwa kuwa akianza kuivaa nyumbani mbele ya mume wake ataanza kidogo kidogo kutoka nayo na nakadhalika ilihali si katika mavazi ya wanawake. Ni katika mavazi ya baadhi ya wanaume. Asiivae, nani anayedai [inajuzu] kuivaa mbele ya mume? Si pambo, si katika mavazi ya mapambo. Kinachotakiwa ni yeye ajipambe mbele ya mume wake, na suruwali si katika mavazi ya mapambo.

  • Mhusika: Imam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Y___g7QRKNs&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 07/09/2020